Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa
kivita ICC imeitaka Afrika Kusini kumkamata rais wa Sudan Omar Al-Bashir
ambaye anaripotiwa kusafiri kwenda nchini humo kuhudhuria mkutano wa
Muungano wa nchi za Afrika ambao unaanza leo Jumapili.
Kwenye
taarifa yake , ICC ilisema kuwa waranti mbili za kumkamata Bashir bado
ziko. Anatafutwa na mahakama ya uhalifu wa kivita kuhusiana na uhalifu
ulitokea katika jimbo la Darfur na anakabiliwa na kesi inayohusiana na
uhalifu wa kivita na mauaji ya halaiki.Kama mwanachama cha ICC, Afrika Kusini inastahli kumkamata Bashir ikiwa atasafiri kwenda nchin humo . Lakini Muungano wa Afrika umekataa kushirikiana na mahakama hiyo ya kimataifa ukisema kuwa ICC inawaonea viongozi wa Afrika
