Jun 29, 2015

UCHAGUZI WA WABUNGE WAFANYIKA BURUNDI LICHA YA UPINZANI KUSUSA



Zoezi la upigaji kura nchini Burundi.
UCHAGUZI wa wabunge unaendelea nchini Burundi licha ya maandamano na ghasia dhidi ya uamuzi wa Rais Pierre Nkurunziza wa kutaka kuwania muhula wa tatu.

Baadhi ya vituo vya kupigia kura vilifunguliwa kwa kuchelewa baada ya maguruneti kurushwa.
Upinzani umesusia uchaguzi huo huku Muungano wa Ulaya ukieleza kuwa uchaguzi huo utazidisha mgogoro uliopo.
Umoja wa Afrika (AU) umekataa kutoa waangalizi ukisema kuwa baadhi ya masharti yaliowekwa hayajaafikiwa kwa uchaguzi kuwa huru na haki.

Rais Pierre Nkurunziza.
Zaidi ya watu 70 wameuawa tangu mgogoro huo uanze huku takribani watu 130,000 wakilitoroka taifa hilo.
Chanzo: BBC