Jun 28, 2015

Thea Atetea Chipukizi

Ndumbangwe  Misayo  ‘THEA’ ametaka  wasanii  chipukizi  wathaminiwe  katika  fani  hiyo  kwani  wana umuhimu wao katika  utengenezaji wa Filamu pia.       
Akizungumza  na  safu  hii  katikati  ya  wiki,  Thea  alisema  kila msanii ana  thamani  yake  kutokana  na nafasi yake katika kazi ya Filamu . Hivyo ametaka wathaminiwe  kulingana na kazi zao  badala  ya  kuwawekea  vizuizi vinavyokwamisha  maendeleo  ya  vipaji  vyao .   
"MIMI nimeshirikishwa katika Filamu  na  wasanii  ambao  hawana  nafasi  na  nimeona  kazi zao  ni nzuri  kuliko  hata  hao  wasanii  ambao  wanajulikana  hapa nchini", alisema Thea.