Jun 17, 2015

Serikali ya muungano Palestina kuvunjika

Rais wa Palestina amesema kuwa serikali ya muungano kati yake na wanamgambo wa Hamas itavunjika.
Bwana Mahmud Abbas ameliambia vuguvugu lake la Fatah, kuwa lazima uhusiano huo uvunjike kwa kuwa Hamas haitairuhusu serikali yake kuendesha shughuli katika eneo la Gaza, ambako wameshikilia wao.
Serikali hiyo iliundwa mwaka uliopita na ilitarajiwa kumaliza uhasama kati ya makundi hayo mawili lakini malengo yake yamekumbwa na matatizo mengi.
Hamas wanaongoza Gaza ilhali kundi la bwana Abbas la Fatah limeshikilia maeneo ya wa Palestina ya West Bank.

BBC