Benki za Switzerland zimeripoti
shughuli zisizoeleweka zilizokuwa zikiendelea katika akaunti za benki za
shirikisho la soka duniani FIFA kulingana na mwanasheria mkuu wa taifa
hilo.
Michael Lauber amesema kuwa afisi yake ilikuwa ikichambua
idadi kubwa ya data ya FIFA iliopatikana katika uchunguzi wake wa
ufisadi katika shirikisho hilo.Amesema kuwa huenda akamhoji rais wa shirikisho hilo Sepp Blatter katika mpango wa uchunguzi wake.
Uchunguzi huo unaweza kusababisha kufunguliwa kwa mpango wa zabuni wa michuano ya kombe la dunia la mwaka 2018 na 2022.
FIFA inakabiliwa na madai ya ufisadi baada ya maafisa wa polisi wa Uswizi kuvamia hoteli mjini Zurich na kuwakamata maafisa saba wakuu mwezi uliopita.
Saba hao walikamatwa kufuatia ombi la idara ya mahakama ya Marekani ambayo imewashtaki maafisa 14 wa sasa na wale wa zamani wa FIFA na washirika wao na mashtaka ya ufisadi.
BBC
