Jun 18, 2015

Msajili wa vyama vya siasa ataka kufuatwa kwa sheria

Msajili wa vyama vya siasa Jaji FRANSIS MUTUNGI
Wakati tukiwelekea kwenye uchaguzi Mkuu, Msajili wa vyama vya siasa Jaji FRANSIS MUTUNGI amevihadharisha vyama vya siasa kuwa makini na kuzingatia sheria ya gharama za uchaguzi, akisema kuwa wakikiuka wanaweza kuwasababishia wagombea wao matatizo.

Jaji MUTUNGI ametoa tahadhari hiyo mjini DSM wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema ofisi yake imebaini kuwapo kwa ukiukwaji wa sheria unaofanywa na baadhi ya vyama katika mchakato wa uchaguzi unaoendelea hivi sasa.

Jaji MUTUNGI anavitaka vyama vya siasa na waandishi wa habari kutii sheria ya gharama ya uchaguzi ya mwaka 2010, na pia waandishi wa habari kutambua nafasi yao katika jamii.

JAJI MUTUNGI pia ameviagiza vyama vya siasa kuacha kutoa mafunzo ya kijeshi kwa wanachama wake

chanzo: TBC