Mwazilishi
wa Manjano Foundation na Mmiliki wa Shear Illusions,Shekha Nasser
akielezea jinsi bidhaa ya manjano foundation ilivyo nzuri kwa
ngozi katika uzinduzi uliofanyika katika ukumbi wa Diamond
Jubilee,jijini Dar es Salaam jana.
Meneja
wa Usajili wa vipodozi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Grace
Shimela akizungumza katika uzinduzi wa Manjano foundation akizungumza
katika uzinduzi wa bidhaa ya Luvtouch katika uzinduzi uliofanyika katika
ukumbi wa Diamond Jubilee,jijini Dar es Salaam jana.
Mke
wa Waziri Mkuu,Tunu Pinda alimpaka bidhaa ya Manjano Luvtoach katika
Uzinduzi wa Manjano Foundation na bidhaa za Luvtouch iliyofanyika katika
Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam jana.
Meneja
wa Usajili wa vipodozi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Grace
Shimela akimkabidhi jarida ambalo linaonyesha matumizi mbalimbali ya
Manjano Luvtouch Mke wa Waziri Mkuu,Mama Tunu Pinda katika uzinduzi wa Manjano,uliofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam jana.
Baadhi
ya watu walioshiriki katika uzinduzi wa bidhaa ya manjano Foundation
katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam jana.
Na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.
MAMLAKA
ya chakula na dawa wamewataka wananchi kuepukana na kutumia bidhaa za
vipodozi feki , kwani bidhaa hizo zina madhara makubwa kwa mtumiaji.
Hayo
yamesemwa na Meneja wa Usajili wa vipodozi wa Mamlaka ya Chakula na
Dawa (TFDA) Grace Shimela wakati wa uzinduzi kipodozi aina ya Manjano
Luvtouch katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam jana.
Shimela
alisema kuwa wamiliki wote wa bidhaa vya vipodozi wanatakiwa kusajili
bidhaa zao ili wafanye biashara kwa uhuru kuliko kukimbiza na wakaguaji
wa bidhaa na mamlaka ya chakula na dawa.
Nae
Mwasisi wa Manjano Foundation na Mmiliki wa Shear Illusions,Shekha
Nasser alisema kuwa kipodozi cha Luvtouch Manjano ni kipodozi
kinachotumika na rika zote awe mzee au kijana, pia kinatumika kwa
wakati wa joto au baridi na ambapo kinahitajika.
Pia
aliongezea kuwa ameona wanawake wengi wakitumia vipodozi kwa
kutokuzingatia wakati unaofaa, wengi hutumia vipodozi kwa wakati
usiofaa kama kipodozi cha ofisini ni tofauti na sehemu ya sherehe.
“Huu
ni wakati wa kila mwanamke kujiremba jinsi awezavyo kutokana na
vipodozi kupatikana hapahapa nchini ikiwa vipodozi vingi vimekuwa
vikiwaharibu wanawake ila kwa hiki kinafaa kwa kwa ngozi zetu”alisema
Shekha Nasser.