

Waziri
Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Edward
Lowassa akizungumza wakati akiwashukuru wanaCCM wa Mkoa wa Manyara,
waliomdhani ili apate ridhaa ya chama chake kuwania Urais wa Tanzania
kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Lowassa
amepata wadhamini 42, 405 , Mjini Babati Mkoani Manyara leo, Juni 25,
2015.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.

Waziri
Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Edward
Lowassa akipokea fomu ya udhamini kutoka kwa Katibu wa CCM Wilaya ya
Babati Mjini, Daniel Ole Porokwa, leo Juni 25, 2015. Mh. Lowassa amepata
udhamini wa wanaCCM 42, 405 wa Mkoa wa Manyara.

Waziri
Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward
Lowassa akimsalimia Kijana Jacob Jeremiah ambaye ni mlemavu wa miguu,
alipokutana nae nje ya Ofisi Kuu ya CCM Mkoa wa Manyara, iliopo Mjini
Babari leo Juni 25, 2015, wakati akiwa katika ziara ya kusaka wadhamini
watakaomuwezesha kutapa ridhaa ya chama chake kuwania Urais wa Tanzania
kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.