Msafara wa pikipiki na magari mjini Katavi jana
wakati wanachama, mashabiki, wapenzi na wafuasi wa Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (CHADEMA) walipojitokeza kwa wingi kumpokea Katibu Mkuu wa
Chama hicho, Dk. Willibroad Slaa ambaye yuko kwenye ziara ya mikoa ya
Mbeya, Rukwa na Katavi akikagua zoezi la uandikishaji wapiga kura kwa
mfumo wa BVR, kuhamasisha wananchi kujiandikisha kwa wingi kwenye
Daftari la Kudumu la Wapiga Kura huku pia akikagua maandalizi ya chama
kwenda kushinda uchaguzi mkuu mwaka huu.

