Klabu ya Liverpool imemsajili
mshambuliaji wa Brazil Roberto Firmino kutoka klabu ya Hoffenheim kwa
kanadarasi ya miaka mitano itakayogharimu pauni millioni 29.
Mkataba
huo utaandamana na ukaguzi wa kimatibabu ambao utafanyika baada ya
mchezaji huyo kurudi kutoka Chile ambapo amekuwa akiichezea Brazil
katika michuano ya Copa America.Firmino ambaye amefunga mabao 47 katika mechi 151 akiwa katika kilabu ya Hoffenheim atakuwa mchezaji wa pili wa Liverpool aliyeghali mno.
Kilabu hiyo ya Anfield ilimfanya mchezaji Andy Carroll kuwa mchezaji ghali alipojiunga nayo kwa kitita cha pauni milioni 35 kutoka Newcastle mwaka 2011.
