MWIGIZAJI nyota wa kike Bongo Esha Buheti amefunguka kuwa baridi
aliyokutana nayo nchini Uingereza hakutamani kuendelea kubaki London
kwani toka azaliwe hajawahi kukutana na baridi kama aliyokutana na nayo
huku, kwa alitamani kurudi Bongo.
wanasema kuna baridi Iringa sijui Tanga na sehemu nyinginezo lakini
lile la London si baridi bali ni hatari, nilikuwa nimekata tamaa na
kutaka kurudi kwani baridi ilikuwa kali sana,”anasema Esha.
Msanii huyo alikuwa nchini Uingereza kurekodi filamu akiwa na wasanii
wengine ambao walikuwa na Yusuf Mlela, Husna Chobis wakiungana na
wasanii wengine kutoka Afrika Mashariki Naijeria na waishio Uingereza
Esha anasema kwa sababu alikwenda msimu wa baridi hakufurahia kabisa
kwani muda mwingi alishinda ndani.
FC/bongo movies