Staa wa Bongo Movies, Adam Haji ‘Baba Haji’ amemtolea uvivu ‘The King
Of All Bongo Social Media Network’ Lemutuz kutokana na tukio la
udhalilishaji alilolifanya dhidi yake!
Lemutuz ambaye amezoeleka kwa kutoa hisia na mtazamo wake juu ya
mambo mbali mbali mtandaoni, mapema wiki iliyopita alimnanga Baba Haji
kupitia ukurasa wke kwenye mtandao wa instagram akidai kuwa amekuwa
akisumbua kuhusu michango ya harusikiasi cha kubadili staili ya kudai
michango hiyo.
Kutokana na kitendo hicho Baba Haji alishindwa kuvumilia na kuamua
kuandika waraka wa kumjibu kumjibu Lemutuz kupitia mtandao huo huo wa
instagram ambapo wasomaji wengi walimuunga mkono na kumshambulia Le
Mutuz
Waraka wa Baba Haji ulisema hivi;
Harusi ni jambo la kheri sana kwa wenye kujua, yaani kwa
wale ambao Mwenyezi Mungu aliowapa hali ya kulijua hilo! Kiukweli
hatuwezi kubisha kwamba ktk Africa watu sote hushauriana na kuchangiana
kufanikisha fanction (shughuli) na sio Mahari au maulidi ambayo
nimefanya ili kubariki ndoa yangu, na imekuwa kawaida sana kwa miaka ya
zamani kabla kuzaliwa kwangu 1980 na hadi sasa.
Wajinga (Kina Lemutuz) wasiojua wenye hila na gilba na
inda hupotosha sana watu kwakua tu wao wazazi wao walituibia pesa za
mlipa kodi na kwenda kusoma USA au Ulaya na eti wakachukua mila za huko
ambazo ni za kiyunani kwa udhalilishaji dhidi yangu eti nilikusumbua kwa
simu kukuomba mchango na kisha nikabadili style ya kukufuatilia
unichangie mtu mzima ovyo muongo sana wewe huna utu kabisa umejaa nafsi
ya kizembe na ujinga uliopitiliza.
Sidhani kama una akili timamu na sidhani kama unalilinda jina la mlezi wako abilisi wa mguu mmoja chago mtembea upande upande.
Baada ya Baba Haji kuweka waraka huu, maoni ya wasomaji wengi
yalimshambulia Lemutuzi kwa kile alichokifanya na kumtuliza Baba Haji
kwa udhalilishaji aliofanyiwa na mtanzania mwenzake anayejifanya kakulia
Marekani.
Picha: Baba Haji akiwa na mkewake siku ya harusi yao.
KIU
chanzo: Bongomovies.com