
Mwenyekiti
wa
Halmashauri ya
Wilaya ya Kisarawe, Adamu Ng’imba akiwaonyesha waandishi wa habari jinsi
mji wa Kisarawe utakavyojengwa, katika mkutano uliofanyika katika
ukumbi wa Mikutano wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo,kulia ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kisarawe na Katibu mkuu
wa kamati kuu ya Miradi,Mwanamvua Mrindoko na kushoto ni Afisa Mradi wa
Maliasili wa Wilaya ya Kisarawe,Cheyo Nyegele.

Baadhi ya wajumbe wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe
wakimsikiliza Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, Adamu Ng’imba alipokuwa akifafanua namna ya mji wa Kisarawe utakavyojengwa,kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo,ambapo wilaya ya Kisarawe inatarajia kuuza viwanja zaidi ya 291 kwa wewekezaji wa viwand.
wakimsikiliza Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, Adamu Ng’imba alipokuwa akifafanua namna ya mji wa Kisarawe utakavyojengwa,kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo,ambapo wilaya ya Kisarawe inatarajia kuuza viwanja zaidi ya 291 kwa wewekezaji wa viwand.


Baadhi ya wanahabari kutoka vyombo mbalimbali sambamba na Baadhi ya wajumbe wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe wakimsikiliza Mwenyekiti
wa
Halmashauri ya
Wilaya ya Kisarawe, Adamu Ng’imba alipokuwa akifafanua namna ya mji wa
Kisarawe utakavyojengwa,kwenye mkutano uliofanyika katika
ukumbi wa Mikutano wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo.

Baadhi ya wajumbe wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe wakisoma vipeperushi vinavyoeleza namna ya mji wa kisarawe utakavyojengwa.
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
HALMASHAURI ya
Wilaya ya Kisarawe imetangaza viwanja 291 vilivyopimwa kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda katika
Wilaya hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa
Halmashauri hiyo, Adamu Ng’imba amesema Halmashauri ya Kisarawe ina mazingira rafiki
kwa uwekezaji wa viwanda kutokana na maeneo hayo yalivyopimwa.
Ng’imba amesema kuwa mradi wa viwanja hivyo umeshirikisha
wananchi wa maeneo hayo ili kuweza kuondokana na migogoro baina ya wawekezaji
na wananchi ili kuepuka malengo yaliyokusudiwa yasifanikiwe.
Amesema katika viwanja vilivyopo katika mradi wa viwanda
asilimia 63 ya fedha zitazopatikana katika uuzaji wa kiwanja kwa zitakwenda kwa
mwananchi ni katika kuepuka migogoro hiyo. Amesema wawekezaji baada ya kukamilisha taratibu zote za
umiliki wa ardhi ni miaka mitatu kama ameshindwa kuendeleza Halmashauri
itachukua na kuuza kwa mtu mwingine.
Ng’imba
amesema katika kuondokana na migogoro na ujenzi
holela wa Halmashauri imeamua kushirikisha wananchi katika maeneo
husika. Amesema watakaopata maeneo ya uwekezaji katika Halmshauri ya
Kisarawe watapata hati ndani ya siku saba na wananchi ndiyo
watakaonufaika na
mradi huo.