Godfrey Haongo mkufunzi kutoka Open University nchini Tanzania akitoa elimu ya njia ya mtandao.
Head
of India Tanzania Center of Excellence in ICT (DIT), Dr. Amos Nungu
akiwakaribisha wafanyakazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO), wakufunzi pamoja na walimu waliofika
kwenye mafunzo ya elimu kwa njia ya mtandao.(Picha zote na Geofrey
Adroph wa pamoja blog).
Afisa
mipango kutoka UNESCO, Bi Faith Shayo akimkaribisha Ofisa
anayeshughulikia na masuala ya Elimu Kitaifa wa UNESCO, Tumsifu Mmari
(wa kwanza kutoka kushoto) wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya elimu kwa
njia ya mtandao kwa walimu wa vyuo vya elimu
Ofisa
anayeshughulikia masuala ya Elimu Kitaifa wa UNESCO, Tumsifu Mmari
akifungua mafunzo kupitia njia ya mtandao iliyoandaliwa na UNESCO
yaliyofanyika jijini Dar.
Bi.
Eunice Gachoka kutoka Kenya Institute of Curriculum Development
akijitambulisha kwa walimu (hawapo pichani) waliofika kwenye mafunzo ya
kupitia mtandao.
Daudi
Mbona mkufunzi kutoka chuo cha DIT akiendelea kutoa mafunzo kwa baadhi
ya walimu walioudhuria mafunzo ya kupitia njia ya mtandao yaliyofanyika
kwenye chuo cha Dar es Salaam Institute of Technology (DIT) hapa jijini
Dar.
Baadhi ya walimu wanaoshiriki mafunzo hayo.
Na Geofrey Adroph, Pamoja blog
UNESCO imeaandaa mafunzo ya
uboreshaji wa elimu kwa walimu hususani katika somo la Tehama kwa vyuo
mbalimbali vya hapa nchini vinavyotoa elimu ya ualimu. Mafunzo hayo
yaliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO) Tanzania yamefanyika katika chuo cha Dar es Salaam
Institute of Technology (DIT) ili kuweza kuwapa fursa hiyo waalimu wa
vyuo mbalimbali katika ufundishaji na uelimishaji namna ya matumizi ya
Tehama.
Hii inatokana na baada ya mkutano
wa viongozi wa vyuo mbalimbali pamoja na wadau wa elimu wa hapa nchini
Tanzania hivyo kuona kama kuna mapungufu katika masuala la uelewa na
matumizi ya Tehama hasa katika vyuo hivyo.
Baada ya kuona kuna mapungufu hayo
UNESCO waliamua kuanzisha mradi uitwao UNESCO-China Funds in Trust
Project (CFIT) wakishirikiana na vyuo vya elimu hapa nchini Tanzania
waliamua kuanzisha mradi huo kwa malengo makuu matatu ambayo ni
kuboresha elimu kwa walimu wa vyuo vya ualimu, kuweka mafunzo ya walimu
wanapofundisha katika Tehama ili kuendana na mabadiliko ya teknolojia
pamoja na kuwanunulia vifaa vya Tehama ambavyo vitasaidia katika
kufundishia na kujifunzia, Afisa mipango kutoka UNESCO, Bi Faith Shayo
alivitaja vifaa hivyo kwa kuviorodhesha kuwa ni pamoja na kompyuta,
Projecta, na Sola ili kuhakikisha hakuna tatizo la umeme katika
ufundishaji wa masomo hayo .
Kupitia mradi huo wa (CFIT), UNESCO
imeandaa mafunzo ya siku tano kwa walimu wa vyuo vya ualimu kutoka vyuo
mbalimbali vya Elimu hapa nchini Tanzania ili kuongeza ujuzi na ufanisi
katika ukuzaji wa Tehama hasa kupitia kwenye njia ya mtandao na pia
kuendana na wakati kutokana na mabadiliko pamoja na ukuaji wa matumizi
ya Teknolojia
Mafunzo haya yaliyoandaliwa na
UNESCO yanafanyika katika chuo cha Dar es Salaam Institute of
Technology (DIT) kwa ajili ya kuwapa elimu kwa baadhi ya walimu wa vyuo
ili kupata uelewa zaidi juu ya Tehama.
Wakufunzi wa mafunzo hayo ni Daudi
Mboma ambaye ni Mkuu wa idara ya maendeleo ya biashara kutoka (DIT) na
Godfrey Haongo kutoka Open University of Tanzania ambao wanajukumu la
kuwafundisha walimu mbalimbali kutoka vyuo tofauti hapa .
Waalimu tisa kutoka chuo cha
ualimuTabora, waalimu tisa kutoka chuo cha ualimu Monduli , walimu wanne
kutoka chuo cha ualimu Morogoro, mmoja kutoka Shule direct, wawili
kutoka Chuo kikuu cha Nelson Mandela, mmoja kutoka Ngorongoro Waso
District, pia kuna baadhi ya watakao pata mafunzo hayo wanatokea Wizara
ya elimu ambao wanafanya kazi kwa ushirikiano na UNESCO ili kuweza
kufikia malengo ya mradi huo kwa vyuo vya elimu hapa nchini.
Kutokana na kuwa na uelewa mdogo wa
masuala ya Tehama UNESCO wamejipanga kuweza kupambana na kutoa mafunzo
ya kiteknolojia ili kuweza kuboresha matumizi na upatikanaji wa huduma
za kitehama katika taifa la Tanzania kwa kuanzisha mradi huo wa kutoa
mafunzo kwa walimu nao walimu waweze kwenda kuutumia ujuzi huo katika
ufundishaji kwenye vyuo wanavyofundisha ilikuweza kuwapa upeo mkubwa
wanafunzi wa ualimu ambao ndio watakao kuwa kipaumbele katika kufanya
nchi iwe katika mfumo mzuri wa Tehama.