
Daraja
la Rando lililopo Kawe jijini Dar lionekanavyo baada ya kukumbwa na
mafuriko kutokana na mvua zilizokuwa zikinyesha maeneo mbalimbali hapa
nchini na kupelekea usumbufu wa kutokufikika kwa baadhi maeneo ya
ng'ambo ya daraja hilo, tunafahamu kwamba magari mara nyingi ndio
yanasubiana kupishana lakini hapa imekuwa ni tofauti, kwani hapa
Pikipiki (Bodaboda) ndio zinapishana kwa mtindo huo kwa kupita moja
baada ya nyingine.

Hali ni tete katika daraja hilo ambalo lilitengenezwa kwa msaada mkubwa
wa Mbunge wa Jimbo la Kawe, Mh. Halima Mdee, lakini sasa
limepoteza mawasiliano ya barabara kati ya shule ya Sekondari na ya
msingi zilizopo eneo la Rando jimbo la Kawe Manispaa ya Kinondoni
Jijini Dar es Salaam.

Muonekano wa Daraja la Rando ambako halijachukuliwa na Maji.

Maji hayapotei njia na hapa ndipo hupita lakini yameonyeshwa njia ndogo yakajiongeza kutafuta njia zaidi.
picha zote na mtaa kwa mtaa blog