Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma Kapteni Mtaaafu - Chiku Galawa (wa tatu kushoto)
akipokea sehemu ya shuka 422 na godoro 22 yenye thamani ya shilingi
Milioni 10 kutoka kwa Meneja wa NMB Kanda ya Kati - Gabriel
ole-Loibanguti (kushoto). Vifaa hivyo vilitolewa na NMB kwaajili ya
hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma katika hafla iliyofanyika kwenye
kilele cha siku ya wauguzi duniani - Dodoma.
Meneja
wa NMB Kanda ya Kati - Gabriel ole-Loibanguti (kushoto), akikabidhi
sehemu ya magodoro 22 na shuka 422 vyote vikiwa na thamani ya shilingi
Milioni 10 kwa mkuu wa mkoa wa Dodoma Kapteni Mstaaafu - Chiku Galawa
zilizotolewa na NMB kwaajili ya hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.
Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye silele cha siku ya wauguzi Duniani.
Kulia ni Muuguzi Mkuu wa hospitali ya Dodoma - Anatolia Mkindo na
kushoto ni Mganga Mkuu wa Hopsitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma - Ezekiel
Mpuya
BENKI
ya NMB, imetoa msaada wa vifaa mbalimbali kwa hospitali ya rufaa ya Mkoa
wa Dodoma vyenye thamani ya shilingi milioni 10 ikiwa na lengo la
kusaidia uboreshaji wa huduma katika hospitali hiyo kubwa kwa mikoa ya
kanda ya kati – Singida na Dodoma.
Baadhi
ya vifaa vilivyotolewa ni magodoro 22 na mashuka 422 ambayo kwa maelezo
ya mganga mkuu wa hospitali hiyo – Dr Ezekiel Mpuya vitasaidia sana
kuweka mazingira rafiki kwa wagonjwa wanaolazwa hospitalini hapo
hususani akina mama wajawazito na watoto.
habari na michuzi media