May 10, 2015

MBUNGE WA JIMBO LA HAI ATEMBELEA ENEO LA TAMBARARE WILAYANI HAI KUJIONEA ATHARI ZA MAFURIKO NA KUTOA POLE KWA WAATHIRIKA

Mbunge wa Jimbo la Hai  Mhe. Freeman Mbowe akiwa na mkuu wa wilaya ya Hai Mhe. Anthony Mtaka walipotembelea katika ukanda wa Tambarare kujionea athari za mafuriko yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha.
Mbunge Mbowe akiwa na biongozi wengine wa wilaya ya Hai wakitazama miundombuni ya reli ilivyochukuliwa na mafuriko.
Baadhi ya wananchi wakisalimiana na Mbunge Mbowe katika eneo la mafuriko yaliyosomba reli.
Viongozi wa Chama cha mapinduzi wakiwa katika mkutano wa hadhara wa kutoa pole kwa waathirika  wa mafuriko uliofanyika katika kijiji cha Kawaya
Mbunge wa jimbo la Hai Mhe. Freeman Mbowe akiwa ameshika kofia mbili, ya CCM na ya CHADEMA  ambazo alizitumia kuchangisha fedha katika mkutano huo kwa ajili ya wananchi walioathirika na mafuriko katika ukanda wa tambarare wilayani Hai. Picha zaidi BOFYA HAPA