Floyd Mayweather akiwa kwenye bethidei ya Chris Brown.
NEW YORK, MarekaniNI jeuri ya mkwanja! Ndivyo
bondia Floyd Mayweather alivyoanza makeke ya kutumia mkwanja wake baada
ya hivi karibuni kufanya balaa la maana kwenye siku ya kuzaliwa ya
mwimbaji, Chris Brown.
Chris Brown akifungua 'shampeni'.
Hili ni tukio la kwanza kufanywa na bondia huyo baada ya kutoka
kumshushia kichapo mpinzani wake, Manny Pacquiao, Jumapili iliyopita
kwenye Ukumbi wa MGM Grand Arena na kuweka historia ya kuwa bondia
aliyepigana mapambano yote bila kupoteza.
Mayweather, ambaye aliambatana na mpenzi wake, Shantel Jackson na
watu wake wanaounda Kundi la Money Team, walikwenda kujumuika pamoja na
Brown katika siku yake hiyo ya kuzaliwa iliyofanyika kwenye klabu ya
usiku ya Las Vegas 'Super-club Drai's, ambayo ipo ndani ya Hoteli ya
Cromwell.
Mayweather akiwa na totoz.
Mayweather alionekana kutoa kiasi kikubwa cha dola katika mmoja wa
mifuko aliyokuwa ameishika mlinzi wake na kuzitumia kwa kutunza mabinti
waliokuwa wakicheza, huku nyingine akinunulia vinywaji.Hii si mara ya
kwanza kwa bondia huyo wa uzito wa kati ambaye pia anajulikana kama
Money Man kuonyesha jeuri ya fedha zinazopatikana kutokana na jasho
lake.