Mkurugenzi
wa kupunguza umaskini kutoka Wizara ya Fedha, Ana Mwasha (kulia)
akifungua kongamano, linalojadili yaliyojiri katika Malengo ya Millenia
na nini kinastahili kufanywa katika SDG's ili kuhakikisha mafanikio
katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Uchumi na Utafiti wa Kijamii
nchini (ESRF). Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Uchumi na
Utafiti wa Kijamii nchini (ESRF) Dk.Oswald Mashindano na Katikati ni
Naibu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa
(UNDP)- Programme, Amon Manyama.
(Picha na Zainul Mzige wa modewjiblog).
(Picha na Zainul Mzige wa modewjiblog).
Naibu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa
(UNDP)- Programme, Amon Manyama akizungumza kwenye kongamano la siku
moja linalojadili yaliyojiri katika Malengo ya Millenia na nini
kinastahili kufanywa katika SDG's ili kuhakikisha mafanikio
lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Uchumi na Utafiti
wa Kijamii nchini (ESRF).
Sehemu ya washiriki wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa kwenye kongamano hilo.
Alisema
mahitaji ya msingi katika kupunguza umasikini, hayajafikiwa kwani
tumefikia asilimia 28.2 wakati tulitakiwa kuwa asilimia 19.
Alisema
ipo haja kubwa ya kuangalia utekelezaji wa malengo endelevu kwa
kuoanisha na mikakati mingine ya kidunia na ya kikanda, huku kazi kubwa
ikiwa kuhakikisha malengo yote 17 yanatekelezwa katika muda uliopangwa.
Katika kongamano hilo, washiriki walipata nafasi ya kumsikia Balozi
Celestine Mushy kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, akichambua jinsi mataifa yalivyofikia SDGs, michakato
inayoendelea na namna ambavyo anafikiri Tanzania inaweza kunufaika na
mkakati mzima wa maendeleo.
Pia
katika majadiliano, washiriki waliozungumzia haja ya kuangalia takwimu
kwa kuoanisha kwani zimekuwa zikitafutwa na kila mtu mpaka hazijulikani
nani yuko sahihi.
Aidha,
walitaka mkakati wa kiviwanda ndio uzingatiwe kwani ndio unaoonesha
dira ya kufanikisha maendeleo ya kitaifa, kikanda na kibara.
Kongamano hilo liliendeshwa na Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Uchumi (ESRF) kwa ufadhili wa UNDP.
Kaimu
Mkurugenzi wa Taasisi ya Uchumi na Utafiti wa Kijamii nchini (ESRF)
Dk.Oswald Mashindano akizungumza kwenye kongamano hilo.
Pichani
juu na chini ni Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Wizara
ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano Wa Kimataifa Balozi Celestine
Mushy akiwasilisha mada jinsi mataifa yalivyofikia SDGs, michakato
inayoendelea na namna ambavyo Tanzania inaweza kunufaika na mkakati
mzima wa maendeleo.
Dk. Kenneth Mdadila kutoka kitengo cha uchumi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) akiwasilisha mada kwenye kongamano hilo.
Pichani juu na chini baadhi ya wadau walioshiriki kwenye kongamano hilo wakichangia mada kwenye kongamano hilo.
MKURUGENZI wa Kupunguza Umasikini kutoka Wizara ya Fedha, Anna Mwasha
amesema changamoto za uwezo wa kifedha kutekeleza miradi mbalimbali
iliyokuwa katika Malengo ya Milennia, zinatoa ishara tosha ya kubadili
mikakati ili kuwa na mafanikio katika Mipango ijayo ya Maendeleo
Endelevu (SDGs).Alitoa kauli hiyo jana wakati
akizungumza na washiriki wa kongamano, linalojadili yaliyojiri katika
Malengo ya Millenia na nini kinastahili kufanywa katika SDGs ili
kuhakikisha mafanikio.
Alisema ipo haja ya kuimarisha makusanyo ya fedha za ndani na kuacha
kutegemea wahisani, kwa kuwa moja ya sababu za kushindwa kutekelezwa kwa
Malengo ya Millenia ni ahadi za wahisani kutotekelezwa. Alisema
kipengele cha nane katika Malengo ya Millennia, kiligusia ushirikiano
wa kimataifa, ahadi ambazo amesema ukiachia nchi za Luxemburg, Denmark,
Sweden na Norway, mataifa mengi hayakutoa asilimia 0.7 ya pato lao la
ndani, ambalo lilikubalika kimataifa kusaidia Malengo ya Millennia kwa
nchi masikini.
Alisema
ili kuwepo na mafanikio katika miradi mipya na ile inayoendelezwa
kutoka MDGs, iko haja ya kuangalia jamii iliyopo vijijini, ambako
ndiko kwenye umasikini wa kutisha, ingawa Tanzania imefanya vyema
kuondokana na umasikini wa chakula. Umasikini wa chakula umepungua hadi asilimia 9 wakati Malengo ya Millenia yalikuwa ni asilimia 11. Alisema ipo haja ya kufungua mawasiliano ya vijijini, kuinua kilimo, kuwapatia nafasi ya masoko na kuinua huduma za jamii.
Pamoja
na kuzungumzia uwezo wa kifedha, alisisitiza haja ya wadau kuangalia
namna ya kushirikisha sekta binafsi katika kutafuta vyanzo vya fedha kwa
ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ili kukabili umasikini.
habari na michuzi media