
Hivi
ndivyo hali ilivyo katika hili ni Daraja lilalounganisha eneo la Tandale
na Mwananyamala jijini Dar es Salaam, ambapo wananchi wanaokaa maeneo
ya jirani na Daraja hilo waliamua kukusanya viroba vilivyosheheni taka
ngumu na kuwevilundika kwenye kingo za Daraja hilo ili kudhibiti maji
yasiendelee kuchimba njia hiyo. Hali hii imekuja kutokana na mafuriko ya
maji yaliyotokea hivi karibuni katika maeneo mengi hapa jijini kutokana
na Mvua kubwa zilizokuwa zikinyesha.

Hali ilivyo katika mfereji unaopitisha maji katika eneo hilo baada ya kupitiwa na Mafuriko hivi karibuni.

Sehemu ya Magari na watembea kwa miguu wakipita juu ya daraja hilo.
