
Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),Jaji Mstaafu Damian Lubuva
akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,kulia ni
Mkurugenzi Mkuu wa Manunuzi na Logistic,Gregory Kaijage na kushoto ni
Naibu Katibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Mkuu wa Teknolojia ya
Habari na Mawasiliano (Tehama),Sisti Chriati.

Baadhi
ya wandishi wa Habari waliohudhuria katika mkutano wa habari wa Tume ya
Taifa ya Uchaguzi jijini Dar es Salaam leo. (Picha na Avila
Kakingo,Globu ya Jamii.)
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema
uchaguzi mkuu utafanyika kama ulivyopangwa na
haiwezi kufanya uchaguzi huo usogezwe mbele
kutokana na suala hilo kuwa la kikatiba.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini
Dar es Salaam leo, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya
Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu Damian
Lubuva amesema kuwa wanasiasa wamekuwa na
kauli ambazo zinawafanya wananchi wapate hofu
wakati suala hilo kuhairisha uchaguzi halipo
katika tume.
Amesema kuwa wanasiasa wametakiwa kuangalia
maneno ambayo wanayatoa kwani hayana msingi
kwani wanatakiwa watoe sera zao za vyama kwa
wananchi na sio kuisemea tume mambo ambayo
hayana ukweli wowote.
Amesema zoezi la kuandikisha kwa Mkoa wa
Njombe ambalo linaisha kesho na kuhamia katika
mikoa ya Iringa,Lindi,Ruvuma pamoja na Mtwara
ambalo litaanza Aprili 24 mwaka huu.
Lubuva amesema wanatarajia kupokea vifaa vya
kuandikisha kwa kuchukua alama za vidole
(BVR)1600 ambazo zitafanya kazi katika mikoa
hiyo na kuhamia Mikoa ya Dodoma,Mbeya,Katavi
pamoja na Rukwa kuongezeka BVR tena 1600 na
BVR 1,152 zitafanya kazi katika mikoa
Singida,Tabora,Kigoma pamoja na Kagera na
uandikishaji utaanza Mei 2 mwaka huu.
Aidha amesema zoezi la uandikishaji wa daftari la
kudumu la mpiga kura litamalizika Julai mwaka
huu hivyo wananchi wajiandae katika kupiga kura
katika uchaguzi mkuu wa Oktoba.
Jaji Lubuva amesema Rais Jakaya Kikwete anataka
amalize ili apumzike hivyo hakuna mpango
wowete wa kuongeza muda wa uongozi kwake.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii