| .Meneja
Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(kulia)akiongea na waandishi
wa habari(hawapo pichani)wakati wa kuchezesha droo ya 55 ya promosheni
ya Jaymillions inayoendeshwa na kampuni hiyo iliyofanyika leo,ambapo Habibu
Saidi(19)ambaye ni mkazi wa Kabale Bukoba vijijini anayesubiria kuanza
kidato cha tano hivi karibuni kwa kujishindia kitita cha shilingi
milioni 10.Kutoka kushoto ni
Msimamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha,Mrisho Millao na Meneja wa
huduma za ziada wa kampuni hiyo Mathew Kampambe.Ili mteja kujua kama
ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544 au AUTO kwenda namba hiyo iwapo simu haina fedha ambapo mteja akiweka fedha anakatwa shilingi 300/-tu.
Watanzania
wapatao 44 maisha yao yameweza kubadilika kutoka hali ya kawaida na
kuwa mamilionea kutokana na kujishindia fedha taslimu kupitia promosheni
ya siku 100 ya Jaymillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania ambayo
ilianza katikati ya mwezi Februari na inatarajia kufikia ukingoni mapema
mwezi ujao.
Hadi
kufikia sasa wateja wa Vodacom walioshinda wamejinyakulia shilingi
milioni 278 huku mamilioni mengine ya fedha yakisubiri kunyakuliwa na
washindi watakaobahatika katika siku chache zilizobaki kabla ya
promosheni kufikia tamati.
Meneja
Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu amesema promosheni bado
inaendelea na kuwataka watanzania waendelee kuangalia namba zao kama
zimeshinda kwa kutuma neno JAY kwenda namba 15544.
Aliitaja
njia nyingine ya kushinda kuwa ni kutuma neno AUTO kwenda namba 15544
iwapo simu haina fedha ambapo mteja akiweka fedha anakatwa shilingi
300/-
“Promosheni
ya Jaymillions inaendelea hivyo tunawakumbusha wateja wetu kuwa bado
kuna mamilioni ya kujishindia hivyo wachangamkie kwa kujaribu bahati zao
katika siku hizi ambazo promosheni inaelekea ukingoni.
Tunajivunia
kwa kufanikiwa kubadilisha maisha ya baadhi ya wateja wetu walioshinda
wengi wakiwa ni wateja wenye maisha ya kawaida na hii ndio dhamira yetu
kubwa inayoendana na kauli mbiu yetu ya “ukiwa na Vodacom maisha ni
murua”.
Nkurlu
alisema hayo wakati wa kuchezesha droo ya 55 iliyomwibua Habibu
Saidi(19)ambaye ni mkazi wa Kabale Bukoba vijijini anayesubiria kuanza
kidato cha tano hivi karibuni kwa kujishindia kitita cha shilingi
milioni 10.
Baadhi
ya wateja waliobahatika kushinda wanasema kuwa promosheni hii
imewafanya kutimiza ndoto zao zilizoshindwa kutimia kwa muda mrefu kwa
kuwa maisha yao yamebadilika kutoka hali duni kuwa bora zaidi.
Upendo
Madengenya kutoka wilayani Kilolo ambaye alikuwa mhudumu katika nyumba
ya kulala wageni wilayani humo ambaye alijishindia milioni 100
anasema“Jaymillions naifananisha na methali ya Kiswahili ya kulala
maskini ukaamka tajiri kwa kuwa nilikuwa nakabiliwa na changamoto nyingi
za maisha pamoja na familia yangu ,Mungu kaniona nikafanikiwa kushinda
hivi sasa maisha yangu yamebadilikakutoka hali duni kuwa bora na bado
safari ya kuelekea kwenye maisha bora zaidi inaendelea.
James
Mangu kutoka Mwanza ambaye alijishindia milioni 10 anasema kuwa kwa muda
mrefu alikuwa anawaza kupata mtaji wa kuendeleza biashara zake ndogo
ndogo na kwa bahati nzuri ameweza kuibuka na ushindi na kupata mtaji
ambao anakiri kuwa utabadilisha maisha yake na familia yake kwa ujumla
kutoka maisha duni kuwa bora.
Hynes
Petro Kanumba mkazi wa Rukwa anasema:”Katika maisha yangu sitaisahau
Vodacom Kwa kuwa kupitia promosheni yake ya Jaymillions imeniwezesha
kunitoa katika hali duni na kuwa na maisha bora pamoja na familia yangu
na natoa wito kwa watanzania kutozipuuza promosheni hizi kwa kuwa ni za
kweli na zinalenga kutukomboa sisi wanyonge”
Kwa
upande wake Deborah Stanley mshindi wa milioni 10 anasema: “Nimefuatilia
Promosheni ya Jaymillions naona inalenga kuwakomboa kimaisha watanzania
hususani wenye kipato cha chini hasa wajasiriamali wadogo wadogo kama
vile; wamachinga, mama ntilie, wanafunzi na wazee wastaafu ambapo kwa
kiasi kikubwa tunajua watu wa aina hii wanahitaji msaada ili
kujiendeleza kiuchumi. Kwa fedha ambazo baadhi ya washindi tayari
wamezipata wengi zimewasaidia kujikwamua na kujiendeleza kimaisha,"
|