
Vijana
wa Kigoma wakiwa na bango wakimsubiri Mhe. Zitto Kabwe "Mirumbani"
alipokwenda jimboni huko kutoa Ahsante kwa kumchagua kuwa mbunge wao kwa
vipindi viwili
.jpg)
Mhe. Zitto Kabwe "Mirumbani" alipokwenda jimboni huko kutoa Ahsante kwa kumchagua kuwa mbunge wao kwa vipindi viwili
Mbunge
wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe amesema kutimuliwa uanachama na
Chadema ni dhoruba inayomkumba mwanasiasa yeyote anayefanikiwa na kwamba
iko siku atashika “nafasi kubwa ya uongozi ya kuwatumikia Watanzania”
.
.
Zitto
aliwasili mjini Kigoma juzi, ikiwa ni siku chache baada ya Chadema
kutangaza kumtimua uanachama kwa kosa la kupeleka mgogoro wa ndani ya
chama kwenye mahakama.
Alifungua kesi Mahakama Kuu akitaka imuamuru katibu mkuu wa Chadema
kumpa nyaraka za mwenendo wa vikao vya Kamati Kuu vilivyomvua madaraka
yote na baadaye kukizuia chama hicho kumjadili. Hata hivyo mahakama
ilitupilia mbali shauri lake na Chadema ikatangaza mara moja kumtimua.
Akihutubia
mamia ya watu kwenye Kijiji cha Nyarubanda ambako alikabidhi gari la
wagonjwa, Zitto aliwatoa hofu wananchi hao walioonyesha shauku ya kujua
hatma yake na kuwaeleza kuwa hajawatupa, ataendelea kuwahudumia.
“Hakuna kiongozi aliyefanikiwa kisiasa bila kupitia misukosuko ya
kupingwa,” alisema Zitto ambaye anamalizia kipindi cha pili cha ubunge
wake kwenye jimbo hilo.
“Waziri
Mkuu za zamani ya India, Indira Gandhi alifukuzwa na chama chake na
aliamua kuunda chama kipya na baadaye kuwashinda waliomfukuza katika
uchaguzi. Kwa hiyo nawatoa hofu kwa maana ninajengwa zaidi kisiasa.
“Nipo kwenye dhoruba ambayo inanijenga kisiasa na ipo siku nitawatumikia
Watanzania katika nyadhifa kubwa za uongozi.”
Katika
mkutano huo ambao wananchi walimpokea wakiwa na mabango yenye ujumbe
mbalimbali kama “Mheshimiwa Zitto tulikuchagua wewe na siyo chama,” huku
mengine yakiandikwa “chama siyo bora, ubora ni utendaji kazi”.
Viongozi mbalimbali wa CCM na vyama vingine vya siasa walijumuika kwenye
uwanja huo kumpokea Zitto na kushiriki naye kucheza ngoma za asili.
Baadhi
ya viongozi hao ni mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma,
Hamisi Betese, mkurugenzi wa halmashari hiyo, Michael Mwandezi na
viongozi wengine wa serikali za mitaa.
Akiongea
katika hadhara hiyo, Betese alisema kuwa kitendo cha Zitto kutoa gari
ambayo aliwaahidi wananchi kipindi cha uchaguzi ni utekelezaji wa ilani
ya CCM ambayo ndiyo chama tawala.
Aliongeza kuwa yeye kama mwenyekiti wa halmashauri bado anamtambua Zitto
kama mbunge wa Kigoma Kaskazini mpaka hapo taarifa rasmi
zitakapotolewa.
Wanakijiji
hao walishukuru Zitto kwa kutoa gari hilo wakisema litawasaidia kuokoa
fedha nyingi walizokuwa wakitumia kutafuta magari binafsi wanapokuwa na
wagonjwa wanaohitaji matibabu ya haraka.
Mhe. Zitto Kabwe "Mirumbani" akitoa Ahsante kwa wananchi wa jimboni kwake kwa kumchagua kuwa mbunge wao kwa vipindi viwili
Mhe.
Zitto Kabwe "Mirumbani" akiwa amebebwa na wananchi wa jimboni kwake
alipokwenda kuwashukuru kwa kumchagua kuwa mbunge wao kwa vipindi viwili
![]() |
| Mhe. Zitto Kabwe "Mirumbani" akicheza ngoma na wananchi wa jimboni kwake alipokwenda kuwashukuru kwa kumchagua kuwa mbunge wao kwa vipindi viwili |
![]() |
|
Mhe. Zitto Kabwe "Mirumbani" akikabidhi gari la wagonjwa katika kituo
cha Afya cha kijiji cha Nyarubanda jimboni kwake alipokwenda
kuwashukuru kwa kumchagua kuwa mbunge wao kwa vipindi viwili. Kusoma hotuba ya Mhe Zitto Kabwe leo BOFYA HAPA Kwa picha zaidi BOFYA HAPA |




