
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akipata maelezp mafupi namna Tangawizi inavyochakatwa na kusindikwa katika kiwanda hicho,ambapo
Katibu Mkuu Ndugu Kinana alishuhudia kiwanda hicho kukabidhiwa mashine
za kuchakata Tangawizi kutoka SIDO,Kulia ni Mbunge wa Same
Mashariki,Mh.Anne Kilango Malecela.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo mafupi namna Tangawizi inavyosindikwa katika kiwanda hicho,ambapo
Katibu Mkuu Ndugu Kinana alishuhudia kiwanda hicho kukabidhiwa mashine
za kuchakata Tangawizi kutoka SIDO.Kiwanda hicho kilizinduliwa na Rais
Kikwete mnamo Oktoba,2012.Katika taarifa iliyosomwa kiwandani hapo
inaeleza kuwa kiasi cha fedha zaidi ya shilingi bilioni 500 zimetumika
kwa ajili ya ujenzi pamoja na shughuli nyingine za kujenga uwezo ili
kuhakikisha kiwanda hicho kinafanya kazi kwa ufanisi.

Meneja
wa SIDO mkoa wa Kilimajaro Bwa.Daniel Njowero akikabidhi nyaraka za
mashine mpya za kuchakata Tangawizi kwa Mwenyekiti wa Bodi wa Kiwanda
cha Tangawizi,Bwa.Yonaz Yohana Mgonja,huku Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Kinana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakishuhudia

Moja ya shamba la Tangawizi .

Mbunge wa jimbo la Same Mashariki Mama Anne Kilango akizungumza na wapiga kura wake kwenye chuo cha VETA Maore Wilaya ya Same.

Moja ya jengo la chuo cha VETA kilichopo katika kijiji Maore-Same Mashariki ambalo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alikagua na kujionea ujenzi wake,chuo hicho kinafadhiliwa na Kampuni ya Suzuki ya nchini JAPANI

Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza kwenye mkutano mkuu wa jimbo la
Same Mashariki,Ndugu Kinana pia alipokea taarifa ya kazi za chama na
taarifa ya Utekelezaji wa ilani.

Wananchi wakishangilia jambo

Sehemu ya umati wa Wakazi wa Same Mashariki,kijiji cha Ndungu wakishangilia jambo katika mkutano huo wa hadhara.

Mmoja
wa watoto akiwa amebeba kipeperushi cha kumkaribisha Katibu Mkuu wa
CCM,Ndugu Kinana na ujumbe wake ndani ya Jimbo la Same Mashariki

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenyee kijiji cha Ndungu wilayani Same.

Wakazi wa Same Mashariki,kijiji cha Ndungu wakifuatilia mkutano huo wa hadhara

Sehemu ya umati wa Wakazi wa Same Mashariki,kijiji cha Ndungu wakifuatilia mkutano huo wa hadhara

Mbunge wa jimbo la Same Mashariki Mama Anne Kilango Malecela akimuelekeza jambo Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana walipokuwa wakielekea kuweka mashada
ya maua katika makaburi ya watu 24 waliozikwa katika kijiji cha Mang’a
kata ya Goha Same Mashariki ambao walifariki wakati wa maporomoko ya
milima kutokana na mvua kubwa ilionyesha mwaka 2011.

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kusuka nondo za nguzo
za daraja la Mang’a Myamba wakati alipokagua ujenzi wa Daraji hilo Same
Mashariki mkoani Kilimanjaro.Ujenzi
wa Daraja hilo ni ahadi iliyoitoa Rais Kikwete kwa wananchi wa Same
Mashariki katika suala zima la utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM
ya mwaka 2010

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akivuka kwenye miamba ya mawe
wakati alipokagua ujenzi wa daraja la Mang’a Myamba wilayani Same mkoani
Kilimanjaro.

Mbunge wa jimbo la Same Mashariki Mama Anne Kilango akivuka maji katika daraja la Mang’a Myamba,Same Mashariki

Ujenzi wa daraja la Mang’a Myamba,Same
Mashariki ukiendelea,Ujenzi wa Daraja hilo ni ahadi iliyoitoa Rais
Kikwete kwa wananchi wa Same Mashariki katika suala zima la utekelezaji
wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana , Nape Nnauye na Mama Anne Kilango
Malecela wakiweka mashada ya maua katika makaburi ya watu 24 waliozikwa
katika kijiji cha Mang’a kata ya Goha Same Mashariki ambao walifariki
wakati wa maporomoko ya milima kutokana na mvua kubwa ilionyesha mwaka
2011.

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana , Nape Nnauye na Mama Anne Kilango
Malecela wakisali katika makaburi ya watu 24 waliozikwa katika kijiji
cha Mang’a kata ya Goha Same Mashariki ambao walifariki wakati wa
maporomoko ya milima kutokana na mvua kubwa ilionyesha mwaka 2011.

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na Katibu wa NEC
Itikadi n Uenezi Nape Nnauye wakielekea kwenye kiwanda cha Kusindika
Tangawizi ,mara baada ya kukagua daraja kijijini Mang’a kata ya Goha
Same Mashariki .

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kuponda kokoto wakati
alipokagua ujenzi wa daraja la Mang’a Myamba Same Mashariki.