Sehemu
ya nyumba 40 za gharama nafuu zilizojengwa na NHC eneo la Mrara Babati
mkoani Manyara ambazo zilifumguliwa rasmi na Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi.
.....................................
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi
amehitimisha ziara yake ya kutatua migogoro ya Ardhi katika mikoa ya
Mwanza, Arusha na Manyara na ameweza pia kuweka jiwe la msingi mradi wa
nyumba za gharama nafuu Buswelu Mwanza na kufungua nyumba za aina hiyo
zilizojengwa na NHC katika eneo la Longido Arusha na Mrara Babati. Picha
za ufunguzi wa Mradi wa Mrara na Muungano Saguya-Babati
Mkurugenzi
Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akitoa maelekezo kwa watendaji
wake muda mfupi kabla ya ufunguzi wa nyumba za gharama nafuu
zilizojengwa na NHC eneo la Mrara Babati mkoani Manyara
Kikundi
cha sanaa kikiburudisha halaiki ya wananchi( haiku pichani)
iliyohudhuria ufunguzi uliofanywa na Waziri Lukuvi wa nyumba za gharama
nafuu zilizojengwa na NHC eneo la Mrara Babati mkoani Manyara.
Mkurugenzi
Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akionyeshwa mipaka ya eneo
linalomilikiwa na NHC na Msimamizi wa Mradi wa NHC Mrara Babati Bi Linda
Kasilima baada Mkurugenzi Mkuu kubaini kuwepo kwa uvamizi wa baadhi ya
viwanja vya Shirika. Kufuatia hali hiyo Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.
Joel Bendera ameagiza wote waliovamia viwanja hivyo kunyang’anywa mara
moja na nyumba zao kuvunjwa bila fidia.
Mkurugenzi
Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akimpokea Waziri wa Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi alipowasili
katika mradi wa nyumba za gharama nafuu unaotekelezwa na NHC ambapo
aliifungua rasmi baada ya kukamilika. Nyjmba hizo 40 sasa zinauzwa kwa
wananchi mbalimbali wa Babati na nje ya Wilaya hiyo wanaohitaji.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi
akivishwa skafu na skauti kuashiria alama ya amani, upendo na mshikamano
mara alipowasili kufungua rasmi nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na
NHC eneo la rara Babati.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi
akitambulishwa na Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu Msimamizi
wa mradi wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC eneo la Mrara
Babati Bi. Linda Kasilima alipowasili kufungua rasmi nyumba hizo.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi
akifunua kitambaa kuashiria ufunguzi wa nyumba za gharama nafuu
zilizojengwa na NHC eneo la Mrara Babati. Nyumba hizo zimeshakamilika na
zinauzwa kwa wananchi wanaohitaji wa Bbati na nje ya Babati.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi
akikata utepe kufungua nyumba iliyotayarishwa kuwakilisha ufunguzi rasmi
wa nyumba 40 za gharama nafuu zilizojengwa na NHC eneo la Mrara Babati.
Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Joel Nkaya Bendera, Mbunge
wa Babati Vijijini Mhe. Jituson Vrajilal na Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw.
Nehemia Mchechu .
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi
akitoka katika nyumba ya mfano aliyoifungua baada kukagua vyumba na
ubora wa nyumba zilizojengwa na NHC eneo la Mrara Babati.
Mkurugenzi
Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akitoa maelezo ya mradi kwa Mhe.
Waziri wa Ardhi na halaiki ya wananchi wa Babati(hawapo pichani)
waliohudhuria sherehe za ufunguzi wa nyumba za gharama nafuu
zilizojengwa na NHC eneo la Mrara Babati.
Sehemu
ya halaiki ya wananchi waliohudhuria ufunguzi wa nyumba zilizojengwa na
NHC eneo la Mrara Babati uliofanywa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi.
Mkuu
wa Wilaya ya Babati Bw. Crispin Meela akisalimia wananchi na
kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Manayara kusalimia wananchi katika sherehe
za ufunguzi wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC eneo la Mrara
Babati.
Mkuu
wa Mkoa wa Manyara Mhe. Joel Bendera akihutubia wananchi na kusisitiza
maafisa ardhi na mipango miji kufuata sheria katika usimamaizi na utoaji
haki za ardhi Mkoani humo wakati wa sherehe za ufunguzi wa nyumba za
gharama nafuu zilizojengwa na NHC eneo la Mrara Babati.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi
akihutubia wananchi na kusisitiza Halmashauri za Wilaya kutenga ardhi
kwa ajili ya kuwezesha NHC kujenga nyumba nafuu alipofungua rasmi nyumba
za gharama nafuu zilizojengwa na NHC eneo la Mrara Babati.
Mbunge
wa Babati Vijini Mhe. Mhe. Jituson Vrajilal akitoa neon la shukrani kwa
NHC kwa kuwezesha Wilaya ya Babati kupata nyumba bora na kusaidia
vijana mashine za kufyatulia matofali huku akichagiza VETA na taasisi
zingine zihusike kusaidia vijana.
Mbunge
wa Viti maalum Paulina Gekul akisalimia wananchi na kumpongeza Waziri
Lukuvi kwa kuacha ofisi ili kusikiliza kero za wananchi hali aliyosema
inafaa kuigwa na Mawaziri wengine.