
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikatisha
kwenye migomba alipokuwa akikagua mifereji ya inayotiririsha maji
kuelekea kwenye mashamba ya ndizi akiongozana na Mh. Agrey Mwanri.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitoka kwenye chumba cha maabara cha hospitali ya wilaya Siha mara baada ya kuyakagua magari matatu ya kubebea wagonjwa.

Sehemu
ya jengo la hospitali hiyo ya wilaya ya Siha kama lionekanavyo
pichani,ambapo Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alikwenda kukagua.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata
maelezo ya bwawa la umwagiliaji la Kishisha kata ya Ivaeny kutoka kwa
mbunge wa jimbo hilo Mh. Agrey Mwanri wakati alipokagua bwawa hilo.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akichukua ndizi
wakati alipowatembelea akina mama wajasiriamali kabla ya kuhutubia
mkutano wa hadhara katika uwanja wa CCM wa wilaya ya Siha.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata
maelezo kutoka kwa akina mama wajasiamali wakimasai wanaojishughulisha
na kutengeneza bidhaa za urembo kwenye mkutano wa hadhara uwanja wa CCM
Siha.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kuzindua ofisi ya CCM wilaya ya Siha, kulia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya hiyo Ndugu Oscar Temu.

Ndugu Kinana akitoka nje ya ofisi hiyo mara baada ya kuweka jiwe la msingi na kuikagua.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipanda mti wa kumbukumbu nje ya ofisi ya wilaya ya CCM Siha.

Mbunge
wa jimbo la Siha Mh. Agrey Mwanri akimpongeza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana mara baada ya hotuba yake katika mkutano huo.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akivalishwa skafu kutoka
kwa vijana wa Chipukizi wakati alipowasili katika shule ya sekondari ya
Nuru wilaya ya Siha, Kutoka kulia ni Mbunge wa jimbo la Siha Mh. Agrey
Mwanri na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM.

Mkuu
wa mkoa wa Kilimanjaro Mh. Leonidas Gama akimkaribisha Katibu Mkuu wa
CCM,Ndugu Kinana alipowasili mapema leo wilaya ya siha.

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na viongozi wengine wa CCM
wakishiriki kazi ya kumimina zege kwenye shule ya sekondari ya Nuru.

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana katikati akikagua daraja la
Embokoi na Mungushi ambalo limejengwa ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya
uchaguzi ya CCM wilayani Siha.

Baadhi ya wananchi waliofurika katika mkutano huo.

Mbunge wa jimbo la Siha Mh. Agrey Mwanri akiwahutubia wananchi katika mkutano huo.

Baadhi ya wananchi akijizuia mvua na viti wakati mkutano huo ulipokuwa ukiendelea.


Wananchi waliendelea kunyeshewa na mvua ili kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati akiwahutubia.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia
wananchi huku mvua ikinyesha hata hivyo wananchi hao waliamua kujikinga
na viti walivyokuwa wamevikalia ili wamsikilize Ndugu Kinana.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana amewasili katika jimbo la Siha,
katika ziara yake ya kikazi yenye lengo la kukagua kuhimiza na kusimamia
utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ambayo katika jimbo la Siha
imetekelezwa kwa asilimia kubwa ikisimamiwa na Mbunge wa jimbo hilo na
Naibu Waziri wa TAMISEMI Mh. Agrey Mwanri.
Akielezea
utekelezaji wa ilani ya uchaguzi katika jimbo hilo Mh. Agrey Mwanri
amesema ilani ya CCM imetekelezwa kwa kiwango kikubwa ambapo vijiji
vyote katika jimbo hilo vina maji safi na salama ya kunywa, Umeme
umefika katika vijiji vyote kinachondelelea ni usambazaji kwa kila
mwananchi, Suala la huduma za afya nalo liko vizuri kwani vimejenga
vituo vya afya karibu kila maeneo na baadhi ya zahanati zinamaliziwa
kujengwa.
Suala
la Elimu wakati mbunge huyo akiinga madarakani Siha kulikuwa na
sekondari moja, lakini sasa kuna sekondari 17 na ufaulu wa wanafunzi
umeongezeka kwa kiwangi cha juu, Maabara zinakamilishwa ambapo mabati
yamesambazwa karibu kila shule ili kukamilisha ujenzi wa maabara hizo.
Akizungumza
katika mkutano huo pamoja na mambo mengine Katibu Mkuu wa CCM amemsifu
Mh. Agrey Mwanri kwa kazi aliyoifanya katika jimbo hilo kwa kufanya kazi
vizuri na kuwaletea wananchi maendeleo na kuwaambia wananchi katika
mkutano huo kwamba kama kiongozi anafanya kazi nzuri hakuna haja ya
kubadilisha viongozi kama mashati, Mwacheni awaleteeni maendeleo.
Katika ziara hiyo Kinana anaongozana na Nape nnauye Katubu wa NEC Itikadi na Uenezi.