Mar 30, 2015

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL, AZINDUA MPANGO WA PILA 1 JIJINI DAR


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Ghariba Bilal akisalimiana na Ofisa mtendaji Mkuu wa kampuni ya Property International Abdulhalim Zahran, alipowasili Hoteli ya Hyatt Regency Dar es salaam kwa ajili ya kuzindua rasmi mpango wa PILA-1 “JENGA KWA MPANGO EPUKA MAKAAZI HOLELA” na Jarida linalotolewa kila wiki Property International Magazine.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Ghariba Bilal akihutubia Viongozi na watendaji wa kampuni ya Property International inayomilikiwa na watanzania wanaoishi Nchini Dubai wakati wa uzinduzi rasmi mpango wa PILA-1 “JENGA KWA MPANGO EPUKA MAKAAZI HOLELA” na Jarida linalotolewa kila wiki Property International Magazine, uzinduzi huo umefanyika jana katika Hoteli ya Hyatt jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Ghariba Bilal akizindua rasmi mpango wa PILA-1 “JENGA KWA MPANGO EPUKA MAKAAZI HOLELA” uzinduzi huo umefanyika jana katika Hoteli ya Hyatt jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Ghariba Bilal akiagana na Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni ya Property International LTD Mr. Mohammed Sharif baada ya kuzindua rasmi mpango wa PILA-1 “JENGA KWA MPANGO EPUKA MAKAAZI HOLELA” katika Hoteli ya Hyatt jijini Dar es salaam.