Akina mama wa Citizen Foundation wakiwa nje ya Hospitali ya Wilaya ya Temeke na walikokwenda kukabidhi magodoro.
Mwenyekiti
wa Citezen Foundation, Lilian Wasira akimkabidhi moja ya magodoro,
Amosi Kabelege ambaye ni Msimamizi Mkuu wa Hospitali ya Temeke.
Mwenyekiti wa Citizen Foundation, Lilian Wasira akimkabidhi maji ya kunywa, Bi. Ashura aliyelazwa hospitalini hapo.
Mganga
mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Temeke, Amani Malima alimshukuru Mwenyeti
wa Citezen Foundation kwa masaada wa magodoro waliotoa hospitalini
kwake jana.
Akina
mama wa Kikundi cha Citizen cha Tabata jijini Dar es Salaam, jana
kilitoa magodoro 50 na katoni 25 za maji na 25 za soda aina ya Cocacola
ikiwa ni kuadhimisha Siku ya Akina mama Duniani.
Akizungumza
wakati akikabidhi msaada huo, Mwenyekiti wa kikundi hicho, Lilian
Wasira alisema wameguswa sana na tatizo la akina mama kujifungulia
sakafuni ndiyo maana wakaona watoe msaada huo.
Lilian
alisema, wameamua kufanya hivyo badala ya kusherehea siku hiyo kwenye
kumbi za burudani huku wenzao wakijifungulia sakafuni.
Mwenyekiti
huyo alisema hawataishia Temeke tu bali wanatarajia kufanya harambee
nchi nzima kuwahamasisha wadau mbalimbali kuhakikisha huduma ya afya
inaboreshwa. Magodoro hayo yana thamani shilingi milioni 2,740,000.
NA JIACHIE BLOG