Mar 29, 2015
Adam Juma awatolea uvivu madirector wanaojitapa kuwa wao wanaweza zaidi
AJ ambaye ni miongoni mwa madirector wa mwanzo wa Tanzania ameandika ujumbe huu kupitia akaunti yake ya Instagram:
“Hizi vita za katika sanaa za kijinga sana, hazileti maendeleo bali chuki tu. Vita kati ya madirector sio jambo lakushangilia hata kidogo, kwani mtu ukiwa wa kwanza wa pili maana yake nini? Mnapoteza urafiki kwa ummaarufu wa siku mbili. Kitu hiki kilifanyika kwa pfunk na mj, then dunga na mapigo then lamar, wako wapi hawa watu ambao ndio mngongo wa mziki. Ukiwaangalia hawa maproducer wote ni wakali ila ujinga ndio umesabisha ubishani usiokua na maendeleo. Tujifunze kupenda na kuangalia style za wenzetu sio kwa lengo lakusema nani ni mkali au nani ni wakwanza, kwa nia hiyo tutakuza sanaa. Sijawahi hata siku moja kufikiria kwamba nimfunike mtu flani au niwe on top, bali nafanya kwa kadri ya uwezo wangu kuwa tafauti mengine nawaachia watazamaji. Sitaki kufananishwa na mtu yoyote yule kwa uzuri wala ubaya, kama hujaelewa nachokifanya nunua camera fanya wewe. Nawaonya nyie mnaogombana mkiwa mmesahau mlipotoka, UMOJA NI NGUVU UTENGANO NI UDHAIFU. Hakuna aliyebora kati yetu wote tunaudhaifu wetu.”
maneno hayo ameyasema adam juma baada ya siku chache tu katika mtandao wa BONGO5 baada ya director mmoja kujitapa kwa kusema.----- kuwa anayenipa changamoto ni Godfather,mtu ambaye hatushei wateja huwezi kuwa challenge yangu mambo yalikuwa kama hivi-
Swali: Ushindani uko vipi kwenye soko kwa kijana kama wewe mpya ambaye unakuja kwenye upande huu- Dullah
“Ushindani ni mkubwa sana kwenye soko, kuna malegend halafu kuna si malegend ila wanafanya vizuri kwa kiasi chao. By the way sio challenge kwangu kwasababu sio focus yangu,” alisema Hanscana.
“challenge inatokea katika kile ambacho unaki focus, ila wao si focus yangu kwahiyo sio challenge yani hawani challenge mimi kabisa. Ambaye mi wanani challenge ni Godfather kwasababu Godfather anashoot video na Diamond na Hanscana anashoot na Diamond, kwahiyo yule mi ni challenge yangu, ananichallenge labda Nicky Campos ambaye anashoot video na Vanessa Mdee na mi nashoot na Vanessa kwahiyo wale ndo wananichallenge kina Moe Musa ambao tunashare nao wateja, mtu ambaye hatushei wateja huwezi ukawa ni challenge yangu.”
CHANZO hapa
