
Katibu Mkuu wa Wizara ya
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Alphayo Kidata (kulia) bakitoa
tathmini ya zoezi la bomoa bomoa awamu ya tatu linaloendelea katika
Manispaa ya Kinondoni jana jijini la Dar es salaam.Kulia ni Muhandisi wa
Manispaa ya Kinondoni Baraka Mkuya.

Baadhi ya waandishi wa
habari kutoka vyombo mbalimbali wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya
Ardhi Bw. Alphayo Kidata (hayupo pichani) alipokuwa akitoa tathmini ya
zoezi la bomoa bomoa kwa wananchi waliovamia maeneo yanayomilikiwa
kisheria na watu wengine katika manispaa ya Kinondoni jana jijini Dar es
salaam.

Moja ya ukuta uliojengwa kinyume cha sheria katika eneo lisiloruhusiwa eneo la Tegeta ukibomolewa jana.

Baadhi ya wananchi katika
manispaa ya Kinondoni wakiondoa bidhaa zo katika maduka eneo la Tegeta
Machakani kupisha zoezi la bomoa bomoa kufuatia maduka hayo kujengwa
eneo lisiloruhusiwa, jana jijini Dar es salaam.

Fundi wa Shirika la Ugavi
wa Umeme Tanzania (TANESCO) akiendelea na zoezi la kukata umeme eneo la
Mikocheni B kufuatia zoezi la bomoa bomoa lililokuwa likiendeshwa na
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Manispaa ya Kinondoni,
jana jijini Dar es salaam.

Tingatinga likiendelea
kubomoa maduka eneo la Tegeta Machakani kufuatia maduka hayo kujengwa
eneo lisiloruhusiwa, jana jijini Dar es salaam.

Askari wa Jeshi la Polisi
wakiwa wameimarisha ulinzi wakati wa zoezi la bomoa bomoa maeneo ya
wazi na yale yaliyochukuliwa kinyume cha sheria kutoka kwa wananchi
wanaoyamiliki kihalali eneo la Mikocheni na Tegeta jijini Dar es salaam.