Mwigizaji Riyama Ally amefunguka kwa kinywa chake kuwa baba aliyezaa
naye mtoto wake wa kike aitwaye Fatma, amempita takriban miaka 10.Riyama
alizungumza hayo alipokuwa akihojiwa katika kipindi kimoja cha TV na
kusema kuwa hakuna chochote kinachohusiana na umri katika suala la
mapenzi kwa sababu ingekuwa kuna tatizo basi kwa upande wake ingekuwa
shida.
“ Jamani sidhani kama kuna uhusiano wowote wa umri katika mapenzi,
mimi nimempita baba mtoto wangu miaka 10 na hata mpenzi wangu wa sasa
naye nimempita hivyohivyo, umri hauna nafasi kabisa kwangu,” alisema
Riyama.
PICHA:Riyama Ally akiwa na baba watoto wake.
