Kuna baadhi ya mastaa wanaojua kuyatumia majina yao, kwani licha ya
kuwa mwigizaji na mtangazaji wa redio, Yvonne Cherry ‘Monalisa’ hafanyi
kazi hizo pekee bali ana kampuni inayobeba tenda mbalimbali katika sekta
za umma na binafsi.
Akizungumza na
Gazeti la Mwananchi,Monalisa alisema kuwa anapenda kufanya mambo yake chinichini ndiyo maana walio wengi hawajui anayoyafanya katika jamii.
Gazeti la Mwananchi,Monalisa alisema kuwa anapenda kufanya mambo yake chinichini ndiyo maana walio wengi hawajui anayoyafanya katika jamii.
Hata hivyo, alibainisha kuwa anafanya kazi katika kampuni zaidi ya
tatu kila siku na anatenga muda wa kuwa na familia yake, hiyo ndiyo
sababu pekee inayomwepusha kufanya mambo yasiyofaa.
“Mambo yangu huwa nafanya kimyakimya siyo lazima upige makelele watu
wakujue taratibu watu watakujua tu lazima, nina kampuni yangu mwenyewe
Sherry Company Limited na sasa hivi ni meneja wa Manday Entertainment.
Hii ni kampuni mpya wa filamu na burudani, tuna studio za audio na video
tunataka pia kuanza na usambazaji wa filamu,” alisema.
Monalisa alisema kupitia kampuni yake ametengeneza filamu nyingi.
“Binti Nusa 1,2,3 nilitengeneza kupitia filamu yangu, mara nyingi
nafanya tenda mbalimbali ingawa sijajitangaza sana,” alisema na
kuongeza: “Inatengeneza vitu mbalimbali katika sekta za umma na binafsi.
Ukiachana na kampuni hizi mbili, nafanya kazi ya utangazaji na pia
tamthilia na filamu, niko bize kwa kweli.”
Kuhusu tasnia ya filamu, Monalisa alisema hakuna elimu ambayo haijatolewa kuhusu maisha ya kupendana kwa wanasanii.
“Tumeshahubiri umoja, watu tupendane kwangu mimi naona hapa kila mtu
afanye kwa nafasi yake ili tufikie mahala tunapopataka,” alisema
Monalisa na kuongeza: “Kuwa wasambazaji ni lazima kuwa makini na
masilahi ya msanii mmoja mmoja.
“Wasambazaji nao wanataka kulifanya soko letu liwe gumu, nilikuwa
kinyume na wao, namshukuru Mungu wizara ilishatoa tamko kuhusu bei ya
filamu iliyopangwa na kampuni ya kusambaza filamu ya Steps kwamba
isitishwe.
Filamu hazitauzwa tena Sh1,500, natumaini wataendelea na msimamo wao
huohuo na watakuja na bei elekezi ili sote tufahamu kitakachokuwa
kikiendelea.
bongomovies.com
bongomovies.com
