Hatahivyo Bafana Bafana imeshinda mechi moja kati ya mechi 12 katika mashindano haya ,ijapokuwa haijashindwa katika mechi tano kufikia sasa tangu ianzishe kampeni zake za kufuzu kwa dimba la mataifa ya Afrika mwaka uliopita.
Nayo timu ya Algeria kwa jina maarufu 'The desert warriors imepata sare moja na kupoteza mechi 4 kati ya tano katika mashindano ya mataifa ya Afrika tangu ushindi wao maarufu wa mabao 3-2 dhidi ya Ivory Coast mwaka 2010.
Katika mechi 3 zilizochezwa kati ya mataifa haya mawili ,algeria haijawahi kushinda mechi hata moja.
Je, unatabiri nini katika mechi ya leo? kwa maoni yako basi Ingia katika mtandao wetu wa facebook katika bbcswahili.