
Baadhi
ya walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya maskini katika shehia ya Mpapa
mkoa wa Kusini Unguja wakishiriki katika kazi ya uchimbaji wa mtaro wa
maji kupitia Mpango wa ajira za muda ambao huwawezesha walengwa kulipwa
fedha .
.png)
Mtaro
wa maji uliochimbwa na walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya maskini
katika shehia ya Mpapa wilaya ya Kusini Unguja inayotekelezwa chini ya
mpango wa ajira za muda kupitia TASAF.
.png)
Mmoja
wa walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya maskini wa TASAF katika shehia
ya Mpapa wilaya ya Kati Mkoa wa kusini Unguja akishiriki kazi ya
kuchimba mtaro wa maji.
WALENGWA WA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI UNAOTEKELEZWA NA TASAF WACHIMBA MTARO WA MAJI KUPITIA UTARATIBU WA AJIRA YA MUDA KATIKA SHEHIA YA MPAPA,MKOA WA KUSINI UNGUJA.
Maelfu
ya wakazi wa shehia ya Mpapa wilaya ya Kusini Unguja wanatarajiwa
kunufaika na huduma ya maji safi na salama baada ya kukamilika kwa mradi
wa maji unaotekelezwa na walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya maskini
unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF kwa utaratibu wa ajira ya muda PWP.
Wakizungumza katika eneo la mradi baadhi ya walengwa hao wameonyesha utayari wao katika kuchimba mtaro huo huku wakiipongeza serikali
kupitia TASAF kwa kubuni utaratibu huo ambao wamesema licha ya
kuwaongezea fedha lakini pia utapunguza kero ya upatikanaji wa maji
katika eneo lao .
Chini
ya utaratibu wa ajira za muda ,walengwa kutoka kaya maskini huibua
miradi katika eneo lao na kuitekeleza na kisha kulipwa ujira ikiwa ni
mkakati wa TASAF wa kuziongezea kaya maskini kipato kwa kukidhi mahitaji
muhimu hususani katika Nyanja za elimu,afya,lishe na uchumi, ambapo kwa
mujibu wa utaratibu asilimia 75 ya fedha ni malipo kwa walengwa wakati asilimia 25 ni kwa ajili ununuzi wa vifaa .
Mpango
wa ajira za muda utatekelezwa nchini kote wakati wa kipindi cha hari au
kipindi kigumu kama wakati wa ukame au mafuriko kupitia Mpango wa
Kunusuru kaya maskini,PSSN ambao umebuniwa na serikali
kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF na unatarajiwa kuhudumia kaya
maskini zipatazo laki tisa na ishirini elfu nchini kote kazi
ianayotarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Marchi 2015.
ifuatazo
ni picha za baadhi ya wananchi wa shehia ya Mpapa mkoa wa Kusini Unguja
wakishiriki katika kazi ya kuchimba mtaro wa maji kupitia utaratibu wa
ajira za muda.
JIACHIE BLOG