Rais mteule Beji Caid Essebsi kuapishwa kama rais mpya wa Tunisia baada ya kuibuka mshindi katika uchaguzi wa urais nchini Tunisia
Rais mteule wa Tunisia Beji Caid Essebsi anatarajiwa kuapishwa baada ya kushinda uchaguzi wa kwanza uliokuwa huru nchini humo.
Alimshinda rais aliyekuwa mamlakani Moncef Marzouk.
Ushindi wake unaaminisha kwamba Tunisia ndilo taifa ambalo limejinasua kutoka utawala wa kiimla hadi ule wa kidemokrasia.
Siku ya jumatatu,tume ya uchaguzi ilithibitisha kuwa bwana Essebsi alishinda kura ya raundi ya pili dhidi ya Marzouk.
Rais huye mteule ataapishwa katika bunge la wawakilishi wapwa ambapo chama chake Nidaa Tounes kimepata wabunge wengi.

