Shirika la Umoja wa mataifa
linalowashughulikia wakimbizi linaloungwa mkono na mashirika zaidi ya 30
ya kibinaadamu, limeyaomba mataifa yote duninai kuwakubali wakimbizi
zaidi walioathirika na vita vya kiraia nchini mwao.
Shirika hilo
la UNHCR limeandaa mkutano leo mjini Geneva ambapo nchitajiri kutoka eneo nje ya eneo hilo zitaombwa kuwapokea angalau wakimbizi laki moja na elfu 30.
Zaidi ya watu milioni tatu wamekimbia Syria karibu wote wakiwa wanaishi katika kambi za wakimbizi katika mataifa jirani.
Mpaka sasa ni maefu kidogo ya wakimbizi waliopata hifadhi Ulaya au Marekani.
Wito huo kwa nchi tajiri kukubali asilimia 5 ya wakimbizi hao ina maana kuwapokea wakimbizi laki moja na elfu 80 wanawake na watoto au watoto walio peke yao wakiwa ndio wengi wa walio katika hatari kufikia mwisho wa mwaka ujao.
Lakini serikali nyingi na Umoja a mataifa zinaona kama kuwapa makaazi mapya wakimbizi hao kuwa hatua ya mwisho isiyo bora- inadhaniwa kwamba kila wakimbizi wakiwa karibu na nyumbani basi ndipo kunapokuwa na uwezekano wao kurudi.
BBC swahili.com
