MWIGIZAJI mahiri Riyama Ally, amesema baada ya kuigiza filamu nyingi
za watu, safari hii ameamua kuonyesha upande wake wa pili baada ya
kuandika muswada wa filamu yake mpya iitwayo ‘Msuto Daily’.
Riyama ameelezea filamu hiyo ambayo tayari imeshapelekwa
sokoni, kuwa ni kazi ya mikono yake ambapo amejitahidi kuonyesha ubunifu kwa lengo la kushibisha soko lake.
sokoni, kuwa ni kazi ya mikono yake ambapo amejitahidi kuonyesha ubunifu kwa lengo la kushibisha soko lake.
“Msuto Daily ni kazi ya mikono yangu, nimetunga stori na kucheza kama
mhusika mkuu. Ni filamu ya Kiswahili na imechezwa uswahilini haswaa,
chezea vyumba sita wewe. Humu ndani umbea kwa kwenda mbele hasa
ukiujulia maana umbea kipaji, mashabiki wanaweza kupata nakala zao
sehemu wanazouza CD maana kazi ilishatoka,” alisema mwigizaji huyo.