Koleta alisema kwa sababu uchawi hauna ushahidi si rahisi kutamka
hadharani lakini yeye anathubutu kusema ukweli kuhusu jambo hilo.
“Wengi wanaogopa kusutwa lakini lisemwalo lipo na kama halipo laja,
suala la uchawi katika tasnia ya filamu lipo wala watu wasikatae,
unakuta msanii anajua kuigiza lakini akipewa nafasi ya kufanya hivyo
haonekani anafichwa,” anasema Koleta.
Msanii huyo anawataja baadhi ya wasanii ( majina tunayahifadhi) ambao
hadi sasa wana uwezo mkubwa katika kuigiza lakini hawatambi na hawana
hamu ya kuigiza tena kutokana na kufanyiwa mchezo mchafu.
“Kwanza hawapewi nafasi pamoja na uwezo wao mkubwa, wanaopewa nafasi
ni wale waliojiweka sawa,” alisema Koleta na kuwataka wasanii kuwa
makini katika tasnia hiyo.
