Mwigulu Nchemba akiwasili Uwanja wa MKutano Geita mjini jana.
Mapokezi ya Naibu Katibu Mkuu CCM Bara, Mwigulu Nchemba yakiendelea kwa shamrashamra za kutosha.
Hisia za Wananchi kwa Mwigulu Nchemba ambaye katika Bango moja wapo anasomeka kama SOKOINE WA PILI NCHINI TANZANIA.
Sehemu ndogo tu ya Maelfu ya Wananchi waliofika Kumsikiliza Mwigulu Nchemba.
Mwigulu akikaribishwa Geita kwa Mabango.
Kiongozi wa ACT Kanda ya
Ziwa(Mratibu) akitoa shukrani zake za dhati kwa Mwigulu Nchemba kwa
namna alivyokuwa mfano kwa kutetea Masikini na Wanyonge ndani ya BUnge
na Nje ya Bunge.
Mkuu wa Mkoa wa Geita akisalimia wananchi.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa
Geita Ndugu Msukuma akizungumza na Wananchi wake kuhusu Kero mbalimbali
zinazowakumba ndani ya Mkoa wa Geita,Kubwa likiwa Wazawa kutopewa
kipaumbele kwenye Madini, Pia unyanyasaji kwa Wachimbaji wadogo.
Comrade Mwigulu Nchemba wakiwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita wakati wa Mkutano jana.
Tanzania Oyeeeeee,Hiyo ndio salamu ya Mwigulu Nchemba mara zote apandapo Jukwaani kuzungumza na Wananchi.
"Uchaguzi wa Serikali za
Mitaa hatujazi nafasi,Tunatafuta viongozi wenye uwezo wa kusimamia
Halmashauri zetu za Vijiji, Mitaa na Vitongoji ili ziweze kufanya kazi
za Maendeleo kwa Uadilifu na Ufanisi wa hali ya Kuridhisha"
Hii ni sehemu tu ya
Maelfu ya Wananchi wa Geita waliofika Kusikiliza Ujumbe wa Naibu Katibu
Mkuu CCM Bara Mwigulu Nchemba,Kuhusu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na
Kero za Wananchi wa Geita.
Mwigulu Nchemba
akiwasisitiza Wananchi kuchagua wagombea wa Chama cha Mapinduzi
kwasababu ndio wenye sera inayotekelezwa,Hivyo wanajua mahitaji ya
Wananchi wao.
"Kuna Wananchi wanatamani
sana kubadirisha Vyama kama Nguo,Kubadirisha vyama sio suluhisho la
Kutatua kero za Maendeleo.Tujitahidi kufanya maamuzi yenye tija wakati
wa uchaguzi,tuchague Viongozi imara na wenye nia ya kuwaongoza.Achaneni
na kubadirisha vyama vya siasa"
Kupanga ni Kuchagua
Naibu katibu Mkuu
akisisitiza kuwa hakuna atakaye ichafua Tanzania yeye akabaki
salama,Hakuna atakaye Iba mali ya Umma akatembea kifua mbele.Wahujumu
Uchumi wote wa Nchi hii waanze kujiandaa kisaikolojia.
Muonekano wa Umati wa Wananchi waliotulia wakisikiliza hoja za Msingi kutoka kwa Mwigulu Nchemba.
Comrade Mwigulu Nchemba akisisitiza Jambo kwa Wananchi wa Geita Mjini kuhusu Uchaguzi wa serikali za Mitaa.
Sehemu ya Wananchi wakati wa Mkutano huo.
Comrade Mwigulu Nchemba akiagana na Wananchi wa Geita Mjini.
MKutano Umeshamalizika na Wananchi wanarejea makwao