Dec 8, 2014

MAMA KANUMBA: Skendo ya Kanumba iliyonitesa ni ya Ung'eng'e

Mama wa marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa  ambaye kwasasa  ameingia kwenye tasnia ya filamu hapa nchini  amefunguka kuwa hakuna skendo ambayo ilimsononesha kama ile ya mwanaye huyo kuambiwa hajui Kiingereza .


Mama Kanumba alifunguka hayo juzikati katika mahojiano maalum na Mwandishi Wetu : “Eti Kanumba hajui Kiingereza , hili lilinishtua sana nikalipinga kwa nguvu zote sababu najua mwanangu hata shule alikuwa kichwa, ” alisema mama Kanumba .

Skendo ya kudaiwa kutozungumza Kiingereza kibovu iliibuka mwaka 2009 katika Jumba la Big Brother Afrika Kusini wakati Kanumba alipoalikwa kutembelea mjengo huo.
Mama kanumba ameshaingia kwenye sanaa ya uigizaji na ameshafanya kazi nzuri kwenye filamu iitwayo MAPENZI YA MUNGU ambayo ameigiza na mastaa kadhaa akiwemo Elizabeth Michael aka Lulu na mwanamziki Linnah Sanga.

Bongo movie.com