Akizungumza na gazeti la Uwazi, Mainda alisema kuwa ndani ya tasnia ya filamu bado mambo ni magumu kwani mastaa wengi wamekuwa nyuma na matendo ya Mungu kwa kufanya anasa kila kukicha huku wengine wakizidi kuchafuana kwa kupigana majungu.
“Ni kweli mwaka umeisha lakini lazima tujue wapi tumekosea, lakini wasanii wetu hawana roho ya kuamini kuwa Mungu yupo ndiyo maana wanapigana majungu kila kukicha.
Tangu kifo cha kipenzi Kanumba kutokea nilisemwa sana na baadhi ya wasanii wakidai kuwa siwezi kuwika tena lakini wanasahau kuwa niko bize na kazi ya Mungu na si kupiga majungu au kukaa kijiweni kumsema mtu,” alisema Mainda.
MUNGU KWANZA JESUS is my Lord and saviour;the ultimate reson for my lifeHayo ndio maneno alioandika kwenye wasifu "BIO" wake wa kwenye mtandao wa INSTAGRAM
NA BONGO MOVIE.COM
