Frola Mbasha pichani kulia akiwa na Mumewe Mbasha wakati huo.
Mwimbaji maarufu wa nyimbo za injili
nchini Tanzania,Flora Mbasha,amekwenda katika mahakama ya hakimu Mkazi
Kisutu jijini Dar-Es-Salaam,akiomba kuvunjwa kwa ndoa yake na mumewe
Emanuel Mbasha.
Flora amefungua kesi ya madai namba 64 ya mwaka huu kesi ambayo inasikilizwa na hakimu mkazi,Devota Kisoka. Flora
anadai kuomba kuvunja ndoa hiyo na apewe talaka ni kutokana na tabia ya
mumewe kumpiga,kumnyanyasa na kushindwa kumpatia matibabu.
Katika
hati hiyo ya madaianaendelea kudai kwamba mgogoro wao waliwahi
kuufikisha kwa ustawi wa jamii,kwa ajili ya upatanishi lakini
ilishindikana wakashauriwa walifikishe suala lao mahakamani.
Flora
anaiomba mahakama itoe talaka,iamuru aendelee kukaa na mtoto,matunzo ya
mtoto yatoke kwa mbasha na wagawane mali walizochuma pamoja.
