
WAUMINI
wa Kislamu nchini wametakiwa kusoma zaidi Quran na vitabu vingine
vinavyoeleza misngi imara ya dhebu hilo na kuyaelewa yaliyomo badala ya
kukimbilia kuhubili mambo ya kidunia na kiutawala ambayo ni kinyume na
inavyoelekezwa.
Kauli
hiyo imetolewa juzi na kiongozi wa Msikiti wa Dhehebu la Wahidi ambao
ni waislam, Mohamed Moridina wakati wa kilele cha kuazimisha sherehe ya
“ASHURA” iliyoambatana na mafunzo na maandamano ya kuzunguka katika
barabara za mtaa wa Libert, Nyerere, Nkuruma na Jaffaries na kisha
kuishia mskiti wa Shia Ithna Ashery Asghery uliopo mtaa wa Nkomo jijini
hapa.
Pia kushiriki kwao katika kusoma
yale yaliyosimamiwa na kiongozi wao Imam Hussein jinsi ya kushinda
dhulma hali ukiwa unadhulumiwa jambo ambalo likifanyika litasaidia
watoto wadogo kutambua misingi na maandiko hayo kwa kuwapeleka kwenye
nyumba za ibada badala ya kuwaacha majubani wakiangalia Tv na kufanya
mambo ambayo yatasababisha wao kupotoka.
Moridna
alisema kwamba kutokana na waumini wengi kujihusisha na vitendo ambavyo
haviendani na maandiko ya vitabu vya dini vimesababisha kuwepo vitendo
viovu ikiwa ni pamoja na ubakaji, kutumia dawa za kulevya, uchochezi na
hata kutumia uhuru wa kukejeri baadhi ya madhehebu ya dini nyingine.


“Tunatakiwa
kuwa na ujasili wa kutetea haki kama Imam Hussein, Marehemu Rais Nerson
Mandela alipokuwa alipokuwa amefungwa gerezani na vingozi
wa serikali ya Makaburu baada ya kuwa jela miaka 20 kwa kukataa kutii
amri ya makaburu hao siku moja alikumbuka yaliyofanya na Imam
Hussein,”alisema.
Aliongeza
kuwa Mandela ghafla alipata kusoma na kukumbuka maneno ya Imam Hussein
katika harakati za Kerbala na kumpa nguvu ya kupambana na makaburu ili
haki ya kuwa huru ipatikane ikiwa ni pamoja na kulikomboa Taifa la
Afrika kusini jambo alilifanikiwa.

Aidha
ameipongeza serikali kwa kusimamia vyema haki na taratibu kwa kutoa
uhuru wa kuabudu kwa madhehebu ya dini mbalimbali pamoja na kushirikiana
na madhehebu hayo kuhakikisha amani na utulivu vinaendelea kuwa nguzo
ya taifa hili.

“Serikali
haina ubaguzi wa dini wala rangi hivyo ni vyema wananchi tukashirikiana
na serikali kudumisha misingi hii ili taifa letu liendelee kuwa na
amani na utulivu uliopo, na kukomesha tabia ya watu wachache wanaotaka
kuivuruga kwa kisingizio cha dini,

Aliongeza
kuwa ukiwepo kubaguana kikabila na rangi zetu ni jambo ambalo likiachwa
kuwepo viashilia hivyo na bila kukemewa na viongozi wa dini, siasa na
serikali litasababisha ufa na kuanza kutowekwa kwa amani
iliyopo,”alisisitiza.

Wito
wangu kwa waumini na wana jamii kushirikiana kupinga na kukomesha
unyanyasaji wa aina yoyote unaofanywa na baadhi ya watu ambao hawataki
kumwamini mungu na kurejea katika maandiko ya vitabu vya mungu na
viongozi wengine wa serikali kutumia mamlaka yao kuwakandamiza wananchi.
![]() |
| Wauminiwa Msikiti wa Dhehebu la Wahidi ambao ni waislam, wakiwa katika maandamanoya kilele cha kuazimisha sherehe ya “ASHURA” wakiwa katika mtaa wa Nyerere jijini Mwanza. |
![]() |
| Maandamano ya kuzunguka katika barabara za mtaa wa Libert, Nyerere, Nkuruma na Jaffaries na kisha kuishia mskiti wa Shia Ithna Ashery Asghery uliopo mtaa wa Nkomo jijini hapa yakiendelea. |
![]() |
| Akinamama na watoto nao walikuwa mstari wa mbele katika sherehe hizo. |
![]() |
| Viongozi mfano wa kuigwa.NA PETER FABIAN, WA GSENGO BLOG, MWANZA. |




