Askofu Beatus
Kinyaiya
Hatimaye
leo baba Mtakatifu Papa Francisco amempandisha kutoka askofu hadi kuwa
askofu Mkuu askofu Beatus Kinyaiya, O.F.M. Cap (pichani) wa jimbo kuu
Katoliki la Dodoma.
Askofu Beatus
Kinyaiya alizaliwa Mei 9, 1957. Akapata daraja takatifu la Upadre
katika shirika la Kimisionari la Wafranciscan Minor tarehe 25 juni,
1989.
Aliteuliwa
kuwa askofu wa jimbo Katoliki la Mbulu tarehe 22 Aprili, 2006,
nakusimikwa/ wekwa wakfu rasmi na Kardinali Polycarp Pengo kuwa askofu
wa jimbo la Mbulu tarehe 2 Julai 2006.
Leo
tarehe 06 Novemba, 2014 ameteuliwa kuwa askofu Mkuu wa Jimbo Kuu
katoliki la Dodoma ambalo nalo limepandishwa hadhi na kuwa jimbo kuu.
Atasimikwa rasmi kuanza utume wake huo mpya katika jimbo hilo mwezi wa Januari, 2015.
Na Frederic M. Gabriel
wa Globu ya Jamii