MCHAKATO WA TUZO ZA WANAWAKE WENYE MAFANIKIO TANZANIA WAZINDULIWA RASMI LEO JIJINI DAR
Rais
wa Taasisi ya kijamii ya Wanawake wenye Mafanikio Tanzania (Tanzania
Women of Achievement ),Bi. Irene Kiwia (kulia) akisisitiza jambo mbele
ya wanahabari (hawapo pichani) juu ya utoaji wa Tuzo za Wanawake wenye
Mafanikio Tanzania ambazo zitafanyika Machi 7,2015 kwa mara ya nne tangu
kuanzishwa kwake, ikiwa na lengo la kuwatambua na kuwapongeza wanawake
ambao wamechangia maendeleo ya nchi katika nyanja tofauti.
Mwenyekiti
wa Tuzo za Wanawake wenye Mafanikio Tanzania (TWAA), Mama Sadaka Gandhi
(katikati) akitoa ufafanuzi juu ya namna Tuzo hizo zitakavyokuwa
zikitolewa na wanaohusika kupewa tuzo hizo,wakati wa mkutano na
wanahabari (hawapo pichani) uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa Hoteli ya
Serena,Jijini Dar es Salaam.Kulia ni Rais wa Taasisi ya kijamii ya
Wanawake wenye Mafanikio Tanzania (Tanzania Women of Achievement ),Bi.
Irene Kiwia na kushoto ni Katibu Mkuu wa Tuzo za Wanawake wenye
Mafanikio Tanzania (TWAA),Bi. Hellen Kiwia. Katibu
Mkuu wa Tuzo za Wanawake wenye Mafanikio Tanzania (TWAA),Bi. Hellen
Kiwia akielezea namna ya wanawake watakavyoshiriki ili kuweza kupata
Tuzo hizo. Sehemu ya Waandishi wa habari waliohudhulia Mkutano huo. Timu
nzima ya Taasisi ya kijamii ya TWA (Tanzania Women of Achievement )
inayoratibu utoaji wa tuzo za Wanawake wenye Mafanikio Tanzania (TWAA)
wakiwa kwenye picha ya pamoja