Nov 4, 2014

KITUO CHA BIASHARA CHA KIMATAIFA (WTC) CHAFUNGULIWA RASMI NEW YORK, MAREKANI


Taswira za Kituo cha Biashara cha Kimataifa, WTC.
KITUO cha Biashara cha Kimataifa, WTC kimefunguliwa rasmi kwa shughuli za kibiashara jijini New York nchini Marekani jana.


Kituo hicho kimefunguliwa baada ya miaka 13 tangu majengo ya awali kulipuliwa katika shambulio la kigaidi lililotokea Septemba 11, 2001.
Majengo ya kituo hicho yana thamani ya dola za Kimarekani bilioni 3.8 na yamechukua muda wa miaka nane kujengwa.