
CHAMA cha Alliance for Change and Transparency (ACT-Tanzania) kimesema kinaingia katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa bila kuungana na chama chochote cha siasa kwa sababu wanaamini itikadi za vyama hivyo haiendani na itikadi yao.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana, Ofisa Mawasiliano na Uenezi Taifa, Karama
Kaila alisema ACT haijaungana katika muunganiko wowote na vyama vingine
kama ilivyo kwa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na
taarifa za kwamba nao wako katika muungano huo ni upotoshaji.
“Kuna
taarifa zimezagaa katika mitandao ya kijamii kwamba na sisi tupo katika
hiyo muungano wao, sisi hatujaungana na chama chochote na tunaingia
katika uchaguzi wa Serikali za mitaa tukisimama wenyewe,” alisema.
Aidha,
alisema ACT itaweza kuingia katika muungano wa kisiasa endapo tu
muungano huo utakuwa ni wa kiitikadi na kifalsafa lakini katika muungano
uliopo ukiwamo ule wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) hauna mrengo
unaofanana na ACT.
Mwenyekiti
wa ACT mkoa wa Dar es Salaam, Hamisi Chambuso alisema katika mkoa huo
chama mpaka sasa kina wagombea 56 katika wilaya ya Temeke, 32 Kinondoni
na Ilala 19 na kwamba ACT itakuwa na wagombea karibu nchi nzima katika
uchaguzi wa Serikali za mitaa ingawa alisema kwamba kwa Mkoa wa Pwani
hawana imani nao