STAA wa filamu Bongo, Halima Yahaya ‘Davina’ amefunguka kuwa yuko katika mateso makali baada ya kuzuiwa kumuona mwanaye kwa takriban miezi mitatu na mzazi mwenzake.
“Hakuna kitu kinachouma kama mtu kunikataza kuiona damu yangu, nimebeba mimba kwa miezi tisa halafu mwanangu hataki nimuone, nashindwa kumuelewa sijui ni kosa gani kubwa nimefanya hadi nistahili adhabu hii,” alisema Davina.