MADAMUUU! Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ amecharuka na kudai anachukizwa kwa kiasi kikubwa na wasanii ambao wanapenda kumfanyia majungu kutokana na chuki zao binafsi
.
“Watu wenye majungu hawanisumbui kichwa kabisa nabaki nawatazama tu, sababu sina maringo wala majivuno kwa mtu yeyote, sasa cha ajabu wengine wanasema naringa, kwa staili hiyo hatutafika mbali maana wasanii wa nchi za wenzetu wana umoja hawana mambo ya aina hiyo,” alisema Wema.