Sep 11, 2014

Wanasayansi wagundua mifupa ya mnyama mkubwa zaidi ya dinosaur aliyeishi Rukwa


la-sci-sn-titanosaur-tanzania-africa-dinosaur--005
Wanasayansi wakiwa kwenye bonde la ziwa Rukwa walipogundua mabaki ya mnyama huyo
Wanasayansi wanaochunguza viumbe vilivyoishi zamani (Paleontologists), kutoka chuo kikuu cha Ohio nchini Marekani, wamegundua mnyama mkubwa zaidi kuliko dinosaur aitwaye Rukwatitan bisepultus, aliyekuwa na miguu ya mbele yenye urefu wa futi 6 1/2 na ambaye uzito wake ukadiriwa kuwa zaidi ya tembo kadhaa
.
Ugunduzi huo uliofafanuliwa kwenye jarida la Vertebrate Paleontology umesaidia kupatikana kwa uhakika wa uwepo wa mabaki ya ‘titanosaur’ barani Afrika ambako wanyama wakubwa aina ya ‘sauropods’ hawakuwa wengi.
Mabaki ya Rukwatitan bisepultus ambayo ni pamoja na mbavu, miguu na mifupa ya kiunoni, ilipatikana kwenye bonde la ziwa Rukwa. Mnyama huyo aina ya ‘titanosaurian sauropod’ alikufa takriban miaka 100 iliyopita.
Wanyama hao wakubwa wanafahamika kwa shingo zao ndefu.

la-sci-sn-titanosaur-tanzania-africa-dinosaur--006
la-sci-sn-titanosaur-tanzania-africa-dinosaur--002
                                             la-sci-sn-titanosaur-tanzania-africa-dinosaur--004
Soma zaidi habari hiyo hapa.